Rais wa Kenya William Ruto, anayetamatiza ziara yake ya siku nne nchini Marekani, amesema, yeye ndiye aliyeamua polisi wa nchi yake kwenda nchini Haiti, na wala sio Marekani.

0:00

4 / 100

Ruto ameitoa kauli hii mbele ya rais Biden, kujibu madai kuwa Kenya, imesukumwa na Marekani kuwapeleka polisi wake zaidi ya Elfu 1 kusaidia kurejesha utulivu jijini Port au Prince.

Kutumwa kwa polisi wa Kenya kuongoza kikosi cha Kimataifa kusaidia kuleta utulivu nchini Haiti, unakabiliwa na upinzani kutoka Mahakamani, kutokana na chama cha upinzani cha Third Way Alliance kupinga mpango huo, unaosema ni kinyume cha Katiba.

Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema nchi yake itahakikisha Kenya inakuwa mwanachama wa jumuiya ya nchi za kujihami za magharibi NATO, hatua ambayo itaifanya Kenya kuwa taifa la kwanza kwenye ukanda wa jangwa la Sahara kuwa mwanachama.

Katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Marekani, rais Ruto, aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea demokrasia na usalama wa ukanda na dunia.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

"DOING MUSIC WAS NOT MY DREAM I...
Nigerian artist Zlatan Ibile has disclosed that he fell into...
Read more
RAIS LAPORTE ASHTAKIWA KWA KULA RUSHWA ...
Michezo Rais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporte, ashtakiwa kwa...
Read more
MAKONDA AITWA KAMATI YA MAADILI CCM
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
RUTO akanusha kuhusika kwenye vifo vya Waandamanaji
Rais wa Kenya William Ruto anadai kuwa hana damu mikononi...
Read more
Muuguzi Akiri Kufanya Biashara ya Ukahaba Mahakamani
Binti wa miaka 23, Lobi Daudi amekiri shtaka lake la...
Read more
See also  SUA YAPONGEZWA KWA MATUMIZI YA BILIONI 74 VIZURI

Leave a Reply