Taarifa zilizopatikana jijini, Dar es Salaam zinasema Young Africans imefanya mazungumzo na nyota huyo lakini ameshindwa kukubali kusaini mkataba mpya kutokana na ofa mbalimbali alizonazo.
Taarifa hizo zimeelendea kueleza kuwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaongoza katika mbio za ufungaji bora Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2023/24, anasubiri kufanya uamuzi mwingine mapema mwezi ujao.
“Aziz Ki akiwa na wakala wake (mama yake), wamefanya mazungumzo vizuri na Young Africans, lakini akawaambia wasubiri, atasaini siku nyingine, aliondoka na mkataba huo na kuahidi atausaini,” kimesema chanzo cha taarifa kutoka Young Africans.
“Uongozi tayari umempa mkataba mpya, lakini bado hajausaini, Aziz Ki anaonekana kuvutiwa zaidi na ofa kutoka Afrika Kusini kwa sababu kuna timu inamtaka, kuna uwezekano akaondoka,” kimeendelea kusema chanzo hicho
“Ofa ambayo Young Africans wamempa si rahisi kwa Aziz Ki aiache, halafu asaini klabu ya hapa nchini, anachelewa kusaini kwa sababu ya ofa za nje ya nchi alizonazo, hakuna klabu ya ndani ambayo anaweza kwenda huko na kuacha ofa yetu,” Kimeleza chanzo kutoka Young Africans