KWANINI AZIZ KI HAJASAINI MKATABA MPYA YOUNG AFRICANS CLUB

0:00

4 / 100

Uongozi wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, umesema unapambana kumshawishi Kiungo kutoka nchini Burkina Faso Stephanie Aziz Ki, ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Taarifa zilizopatikana jijini, Dar es Salaam zinasema Young Africans imefanya mazungumzo na nyota huyo lakini ameshindwa kukubali kusaini mkataba mpya kutokana na ofa mbalimbali alizonazo.

Taarifa hizo zimeelendea kueleza kuwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaongoza katika mbio za ufungaji bora Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2023/24, anasubiri kufanya uamuzi mwingine mapema mwezi ujao.

“Aziz Ki akiwa na wakala wake (mama yake), wamefanya mazungumzo vizuri na Young Africans, lakini akawaambia wasubiri, atasaini siku nyingine, aliondoka na mkataba huo na kuahidi atausaini,” kimesema chanzo cha taarifa kutoka Young Africans.

“Uongozi tayari umempa mkataba mpya, lakini bado hajausaini, Aziz Ki anaonekana kuvutiwa zaidi na ofa kutoka Afrika Kusini kwa sababu kuna timu inamtaka, kuna uwezekano akaondoka,” kimeendelea kusema chanzo hicho

“Ofa ambayo Young Africans wamempa si rahisi kwa Aziz Ki aiache, halafu asaini klabu ya hapa nchini, anachelewa kusaini kwa sababu ya ofa za nje ya nchi alizonazo, hakuna klabu ya ndani ambayo anaweza kwenda huko na kuacha ofa yetu,” Kimeleza chanzo kutoka Young Africans.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Muhammad Mukhbar Rais wa mpito Iran
NYOTA WETU Makamu wa Rais wa Iran, Muhammad Mukhbar anajiandaa...
Read more
Simone Biles won the vault final on...
Biles soared high into the air as she performed her...
Read more
Generation Z Flexes Its Muscle, Forces Kenyan...
The young people known as Generation Z (Gen Z) in...
Read more
Spain and Barca's Yamal wins 2024 Golden...
Barcelona winger Lamine Yamal has won the 2024 Golden Boy...
Read more
HOW TO MAKE YOUR SPOUSE SEXUALLY DESIRES...
LOVE ❤
See also  YOUNGER AFRICANS YATUPWA NJE YA MICHUANO YA CAF
1. ATTEND TO HIS/HER EMOTIONAL NEEDSEmotional connection leads...
Read more

Leave a Reply