Rais wa mabingwa wa nchi Young Africans Sports Club Eng Hersi Ally Said ametoa shukrani kubwa Kwa wanachama na mashabiki wote wa Yanga Kwa mshikamano ambao walikuwa nao mwanzo wa msimu hadi mwisho wa msimu.Eng Hersi Ally Said pia ametoa neno la shukrani Kwa mfadhili wao GHALIB SAID MOHAMMED Kwa moyo wake wa kuisaidia Yanga kwenye nyakati zote klabuni.
Akiulizwa na mtangazaji wa Azam media Gift macha kama Rais wa Yanga unaweza vipi kujigawa kuhudhuria mechi zote za Yanga msimu huu.Rais Eng Hersi Ally Said amesema ni ngumu sana kujigawa haswa ukizingatia na majukumu yangu Binafsi ya kifamilia,Kazi zangu Binafsi ila mmoja wa watu ambao kwangu ndio kama kioo changu cha mafanikio basi ni MOSES KATUMBI mliki wa klabu ya Tp mazembe.
Nilivyokuwa Drc Congo Nilipata nafasi ya kuongea nae na moja ya maneno ambayo alinambia ukiwa kama Rais wa timu na unataka kupata mafanikio basi unapaswa kuacha mambo yako Binafsi na kusimama na timu siyo kwenye mechi tu hadi mazoezini unapaswa kwenda kuhakikisha Kila mchezaji anapaswa kutambua ukubwa wa thamani ya timu ambayo anacheza.
Maneno haya yalinipa sana nguvu na moyo wa kuipambania timu yangu ndio maana unaniona Kila kwenye mechi nakuwepo na hadi mazoezini nakuwa nao wachezaji wangu tunashirikiana vyema kutimiza malengo yetu.