Kocha Mwinyi Zahera alipopewa kazi ya kuinoa Coastal Union moja ya sehemu yenye shida aligundua ni Eneo la Mlinda lango, wakati huo Kipa alikuwa Ndikumana ambaye Zahera hakuona kitu kwake akawaambia viongozi wa Coastal Union kuwa
“natafuta kipa mwingine kutoka Drc ni kipa mwenye CV kubwa na hamuwezi kumlipa pesa atakayotaka hivyo anakuja kusaini mkataba utakaomalizika mwishoni mwamsimu lengo lake apate mechi za kiushindani atafute soko jingine”
PICHA LIKAANZA
Zahera akapiga simu kwa Matampi akamwambia kama anaweza aje Bongo acheze Coastal msimu huu kama atakuwa na performance nzuri atapata timu zenye pesa zaidi watakaoweza kumlipa zaidi
Matampi akapiga Moyo Konde akakubali kutua Coastal kwa mshahara kiduchu tena ni vile pia hana njaa alishapiga hela Saudia na vilabu vya kwao vikiwemo As Vita na Tp Mazembe
Mechi ya kwanza kwa Matampi ikawa Coastal vs Azam fc, Matampi akachoma ile mechi kwakufanya makosa ambayo mpira alioutaka kuupiga mbali ukaishia kwa @feisal194 bila ugumu Zanzibar finest akampelekea moto, Mechi ikaisha moja bila Viongozi wa Coastal Union wakamlaumu sana Zahera umeleta kipa kaisha huyu sio Matampi tunayemjua
Zahera akawatuliza viongozi wake lakini wapi Viongozi wakahisi Zahera kaleta mchongo wakamshusha timu za vijana akafundishe huko timu ikabaki na makocha wasaidizi kabla ya kuletwa David Ouma kutoka Kenya aliyeikuta timu nafasi ya 15 kati ya timu 16 na leo huwenda wakajihakikishia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao
Matampi aliumia sana kuona aliyemleta kakalia kuti kavu sababu yake, akaanza makali yake hadi leo kafungwa goli 19 tu kwenye ligi akiwa kipa wa pili kuruhusu magoli machache kwenye Ligi nyuma ya Djigui Diara aliyefungwa magoli 13 pekee
Leo Matampi anaitumikia Coastal kabla ya kwenda Simba alikosaini miaka 2 kwaajili ya msimu ujao
Kaipeleka Coastal Union kimataifa baada ya kupita miaka lukuki