Israel imeendelea na Operesheni zake za Kijeshi katika Mji wa Rafar Licha ya Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ) Kuiamuru kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi katika mji Huo na Maeneo Mengine ya Ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahau Amesisitiza kuwa Jeshi la Israel Litaendelea na Opereseheni zake huko Gaza
Hivi leo watu Kadhaa wameripotiwa Kujeruhuiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia iliyopo katika shule ya msingi ya Nazla baada ya mashambulizi mengi ya vikosi vya Israel.
Wizara ya Afya ya Gaza imesema watu 46 wameuawa na wengine 130 kujeruhiwa katika kipindi cha Saa 24.
Tangu Shambulizi la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7 ambalo lilihusisha Utekaji wa Askari wanawake wa Israel na Kupelekelea Machafuko ya Gaza Hadi hivi leo watu zaidi ya Elfu Thelathini na Tano wameripotiwa Kupoteza Maisha.
Hata Hivyo Juma Hili Video zinazowaonyesha Mateka hao wakikamatwa Oktoba 7 zimeachiliwa Mtandaoni na Familia za wanajeshi hao wa Israel wakiamini kuwa watoto wao Bado wapo hai na wanashikiliwa na Hamas huko Gaza lengo likiwa ni kujaribu kuishinikiza serikali kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wanamgambo hao ili kuwakomboa wapendwa wao.
Taarifa zinasema Jeshi la Israel lilikuwa na kanda ya video hiyo, hivi majuzi na liliamua kuikabidhi kwa familia za wanajeshi hao.
Wanamgambo wa Hamas wamesema Video hiyo ni ya Kutengenezwa na haiwezi kuthibitishwa huku wakisisitiza kuwa kutolewa kwake kwa wakati huu ni sehemu ya kupotosha taswira iliyopo.