Habari za uhakika ni kwamba Aziz Ki anamaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu ambao unaishia rasmi tarehe 3 Juni baada ya fainali ya CRDB BANK CONFEDERATION CUP pale Zanzibar. Ukweli kutoka Yanga kupitia Meneja wa Habari ni kwamba Master Ki hajaongeza mkataba mpaka sasa na kuna ushindani wa vilabu vya nje ya nchi kumtaka Aziz. Uhakika ni pale Aziz anaposema hajasaini ila anawapa Yanga nafasi ya mwanzo wakichemka ndio ataondoka.
Kinachowashinda Yanga sio kingine ila ni mahitaji ya Aziz Ki kwenye mkataba mpya tu.Habari za uhakika ni kwamba mwamba amewaambia Yanga anataka dola za Marekani ($) 500,000/= kwa miaka 2 na mshahara wa dola ($) 20,000/ kwa mwezi. Anasema wakati wa kusaini anapaswa kupewa nusu ya hela yani dola ($)250,000/
Dola ($)500,000 = na Tshs 1.3B kwa miaka 2 ambapo dola ($) 250,000 = Tsh675M, ambapo mshahara wa $ 20,000 = 54M kwa mwezi.
Ugumu ni pale viongozi wanapofikiria kama watampa huo mzigo je itakuaje pale PACOME ZouaZoua, Max Nzengeli, Yao Yao watakapoongeza mikataba yao msimu ujao? Wanajikuta wanaweza kuingia mtego wa panya kunasa waliomo na wasiokuwemo. Ndio maana unasikia wanasema wanachama wachangie wanajua ukweli kwamba wanachama hawawezi kuchangia kiasi hicho ila wanaamdaliwa kisaikolojia akiondoka kusiwe na kelele.
Kinachoshangaza zaidi ni pale tunapoambiwa Yanga wanaendelea kusikiliza ofa za mchezaji ambaye kimsingi yuko wiki 2 za mwisho za mkataba wake, alishaingia miezi 6 ya mwisho ya mkataba ambapo ana ruhusa kuongea na klabu nyingine na huku Yanga ikipewa taarifa tu wala sio kuombwa idhini, ni kutaarifiwa. Mbappe kuongea na Madrid leo haombi ruhusa ya PSG wala PSG hawawezi kusema wanasikiliza ofa za Mbappe, Yanga wakishindwa Aziz anaondoka kama Free agent tu.