CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU),kimemjia juu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya matamshi aliyoyatoa dhidi ya Mtumishi wa umma wilayani Longido, kikidai kitendo hicho kinavunja heshima ya mfanyakazi,Kudhalilisha na kuvunja hali na morali ya kufanya kazi.

0:00

4 / 100

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo Mei 28 2024,,Mkuu wa Idara ya habari na Uhusiano wa Kimataifa(TALGWU),Shani Kibwasali amesema mtumishi aliyedhalilishwa na Makonda ni mwanachama wao hivyo wao kama chama hakiwezi kufumba macho kama mwanachama anafanyiwa vitendo ambavyo ni kinyume na Sheria,Kanuni,Taratibu ,Miongozo na Maadili ya Utumishi wa Umma.

Amesema TALGWU inatambua kazi kubwa anayofanya Mkuu wa Mkoa huyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo lakini sio kumdhalilisha Mtumishi wa umma .

‘’Siku za hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kuna video fupi imesambaa ikimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Makonda akiwa katika ziara yake wilayani Longido,Video hiyo fupi inaonesha Mkuu huyo wa Mkoa akiwa kwenye mkutano wa hadhara huku akimuhoji Mtumishi wa Umma na kumtolea matamshi ambayo yanavunja heshima ya mfanyakazi ,yanadhalilisha na kwa kiasi kikubwa yanavunja ari na morali ya kufanya kazi,’’amesisitiza.

Chama kinamsihi Mkuu Mkoa Makonda kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pale ambapo anazungumza na watumishi kwani sio busara kutoa maneno ya kashfa na dhihaka kwa mtumishi iwe mbele ya hadhara au pasipo hadhara,’’amesema.

Amesema kwa kitendo hicho,chama kimetoa rai kwa viongozi wa serikali walioaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhudumia na kuwaongoza watanzania kuacha mara moja kutumia dhamana walizopewa kwa kutoa maneno ya kashfa kwa wafanyakazi.

Kibwasali alisema endapo mtumishi amekosea zipo taratibu za kiutumishi za kumchukulia hatua na sio kudhalilisha utu wake na kumvunjia heshima mfanyakazi.

Aidha naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema anawashangaa wanaojitokeza kusema anawadhalilisha watumishi baada ya yeye kuwakosoa wala rushwa na wazembe wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan alidhalilishwa siku kadhaa zilizopita na watu hao wakiwemo wanawake wenzake walikaa kimya na kumuacha yeye (Makonda) akisimama kumtetea Rais.

See also  The approach of a new Premier League season often brings hope, optimism and excitement. But in Chelsea's case, is it already time to worry?

“Nawaambia tena nitawapiga spana na mnapojitokeza tunapata nafasi ya kujua aah kumbe nae huyu yumo, alidhalilishwa hapa Rais wetu, Mwenyekiti wa chama, Mwanadiplomasia namba moja, Mama mwenye familia, katukanwa asubuhi mpaka asubuhi sikusikia kauli ya mtu yoyote, halafu wanaume sisi ndio tulijitokeza kumpigania yule Mama, leo memba mmoja, mla rushwa mmoja, mvivu mmoja mnapigapiga kelele huko eboo, twende kwenye kazi”.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa Arusha aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

POLISI YATANGAZA MSAKO WA MADADA POA VYUONI...
HABARI KUU Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema limeanzisha...
Read more
YOUNG AFRICANS YATAJA SABABU ZA KUMUACHA JOYCE...
MICHEZO Wakati Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wakisaka...
Read more
Meagan Good and Jonathan Majors, announces their...
Famous Hollywood duo Meagan Good and Jonathan have officially announced...
Read more
Kocha Ange Postecoglou ataka watatu Tottenham
MICHEZO Kocha Mkuu wa Kikosi cha Tottenham Ange Postecoglou ameushinikiza...
Read more
Kurasa za Magazeti ya Leo
Dar es salaam, TANZANIA 🇹🇿.
Read more

Leave a Reply