Martial raia wa Ufaransa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Kwenu mashabiki wa Manchester United, ni kwa majonzi makubwa kuwaandikia leo kuwaaga na kusema kwaherini.
“ Baada ya miaka tisa kuwa pamoja katika klabu, wakati umefika wa mimi kuondoka na kufungua ukurasa mpya katika taaluma yangu hii ya Soka. Tangu nilipojiunga klabuni mwaka wa 2015, nimekuwa na heshima kubwa ya kuitumikia jezi hii na kucheza mbele yenu, mashabiki bora zaidi duniani.
“ Mmekuwa mkituunga mkono na kuwa pamoja katika nyakati nzuri na ngumu, mapenzi yenu na uaminifu wenu umeleta na kuibua motisha kwangu. Ningependa kuwashukuru kutoka chini ya moyo wangu kwa kila kitu ambacho mmenifanyia. Sapoti na upendo wenu ni kumbukumbu ambazo zitabaki moyoni mwangu milele.
Nyota huyo aliyesajiliwa kutoka AS Monaco ya kwao Ufaransa ametoa shukrani kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi na wanachama wote wa klabu hiyo.
“ Nashukuru kuwa nami pamoja katika miaka 9 yangu klabuni hapa (Manchester United) Daima itakuwa moyoni mwangu. Klabu hii imeacha alama kwenye taaluma yangu, ninaondoka kuchukua changamoto mpya.
“ Nitaendelea kuwa Shetani Mwekundu (Red devil) na nitafuatilia matokeo ya timu mara zote. Asanteni tena kwa kila kitu na tutaonana hivi karibuni. Kwa moyo wangu wote.”