Bilionea Larry Connor wa Marekani anajipanga kwenda chini ya Bahari kwa kutumia Manowari licha ya ajali mbaya iliyotokea Juni 2023 ambapo watu watano walifariki dunia.
Connor, atasafiri kwa kutumia Manowari yenye uwezo wa kubeba watu wawili, lengo lake ni kufikia eneo yalipo mabaki ya meli ya Titanic iliyozama mwaka 1912.
Muwekezaji huyo amesema “nimenuia kuionyesha dunia kuwa japo bahari ina nguvu kubwa, lakini inaweza kuwa ya ajabu, yenye kufurahisha na kubadilisha maisha ikiwa utaiendea kwa njia sahihi”.
“Manowari tutakayotumia ina teknolojia ya hali ya juu na inaweza kwenda chini zaidi ya yalipo mabaki ya Titanic”.
Katika safari hiyo Connor ataongozana na Patrick Lahey mmoja wa waongoza manowari wenye uzoefu mkubwa duniani na mwanzilishi mwenza wa kampuni ijulikanayo kama Triton Submarines.