Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la amani duniani Kanda ya Tanzania (Universal Peace federation- UPF) kwa miaka miwili baada ya kukabidhiwa na Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika UPF Adama Doumbia.

0:00

5 / 100

Lengo la Uenyekiti huo ni kuhamasisha amani miongoni mwa watanzania bila kubagua dini, Madhehebu, mila, Viongozi wa Chama na serikali, Wabunge na wananchi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia hadi taifa.

Makabidhiano hayo yanefanyika kwenye hafla fupi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na Mashirikisho ya Amani ya dini, madhehebu mbalimbali nchini na Viongozi wa kimila.

Akimkabidhi barua ya utambulisho wa nafasi hiyo ya Uenyekiti Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Afrika UPF kutoka nchi ya Ivory coast Adama Doumbia amesema UPF ni Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) ambayo kazi yake kubwa ni kutangaza na kusimamia amani baina ya watu wa dini zote na makabila yote na nyanja zote ambalo Makao makuu yake ni nchini Korea.

Aidha, Adama ameagiza kuandaliwa kwa sherehe kubwa Maalum ya kumtambulisha Mwenyekiti huyo mpya wa Shirikisho hilo la Amani nchini Tanzania ambaye atakabidhiwa rasmi na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mama Marie Kigalu ambapo Viongozi mbalimbali watahudhuria.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Actress Funke Akindele addressed a critic of...
Renowned Nollywood star and talented filmmaker Funke Akindele has stirred...
Read more
10 RULES OF SEX DURING DATING.
Don't sleep with a woman on the first day of...
Read more
ROLES OF A WIFE TO HER HUSBAND...
LOVE ❤ 10 ROLES OF A WIFE TO HER HUSBAND There...
Read more
Mwalimu Jela kwa Kuruhusu Mwanafunzi Kumlawiti
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa Wilaya ya Tandahimba mkoani...
Read more
CHAMA NA KAPAMA WASIMAMISHWA SIMBA ...
MAGAZETI
See also  Guinea to challenge DR Congo's unbeaten streak in pivotal AFCON match
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye Jamhuri yetu tukufu...
Read more

Leave a Reply