Leo jioni tutajua nani Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Mchuano uko kwa nyota wawili Stephane Aziz KI wa Yanga SC na Feisal Salum wa Azam FC. Mchuano sio mdogo. Kila mmoja ameshafunga mabao 18.
Yanga SC watakuwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi kucheza dhidi ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mchezo huu utafuatiliwa kwa sababu moja tu. Kwa sababu ya Aziz KI. Yanga SC watatamani kuona Aziz KI anafunga mabao katika pambano hili la mwisho.
Mchezo mwingine utamhumusisha Feisal na Azam FC yake. Mchezo huu utachezwa katika Uwanja wa Nyankumbu Jijini Geita.
Azam FC watataka mambo mawili katika pambano hili. Mosi kushinda ili kuyaweka hai matumaini ya kucheza Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika. Lakini pili ni kutamani kuona Feisal anafunga mabao katika pambano hilo.