Sababu kubwa ni kwamba tarehe hizo Baba wa Taifa hilo “Kim Il-Sung” na “Kim Jong-Il” walifariki, hivyo ni onyo kuonesha dalili yoyote ya furaha kama ni siku yako ya kuzaliwa.
“Kim Il-Sung” ndiye Mwanzilishi wa Nchi ya Korea Kaskazini Mnamo mwaka 1948, pia alikuwa Kiongozi Mkuu (Supreme Leader) wa kwanza wa nchi hiyo Kuanzia Mwaka 1948 mpaka Tarehe 8 Julai 1994 alipofariki.
“Kim Jong Il” alikuwa Mtoto wa “Kim Il Sung”, huyu alikuwa Kiongozi Mkuu wa Pili wa Korea Kaskazini mara baada ya Baba Yake (Kim Il Sung) kufariki Mwaka 1994 mpaka Tarehe 17 Desemba 2011 ambapo yeye pia alifariki.
Baada ya Kifo cha “Kim Jong- Il” aliyefuatia kuwa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini ni “Kim Jong Un” (Watanzania wengi wanamfahamu kama “Kiduku”), Huyu ni Mtoto watatu wa Marehemu “Kim Jong Il” pia Mjukuu wa “Kim Il-Sung”
Mwaka 2021 wakati Wananchi wa Korea Kaskazini wanaadhimisha Miaka 10 ya kifo cha Baba yake Kiduku “Kim Jong Il” utawala ulipiga marufuku nchi nzima kunywa pombe, kucheka cheka hovyo wala kuwa na furaha yoyote ile ndani ya siku 11.