0:00
Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametangazwa Mshindi kwenye uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ambapo amemuangusha aliyekuwa anatetea kiti hicho, Mchungaji Peter Msigwa.
Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo May 29,2024 katika Mji wa Makambako Mkoani Njombe yametangazwa usiku huu baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa kupiga kura.
Sugu ameshinda kwa asilimia 51 huku Mchungaji Msigwa akipata asilimia 49 ya kura zilizopigwa.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mshindi ni Frank Mwakajoka ambaye ni Mbunge wa zamani wa Tunduma.
Related Posts 📫
West Ham United winger Mohammed Kudus's ban has been extended...
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda mkoani Mara hapa...
MICHEZO
Licha ya kufungwa mabao 5-0 na Arsenal juzi Jumanne...
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuendeleza vita dhidi...