Kocha wa Young Africans, Miguel Gamondi amejinasibu kuwa mafanikio waliyoyapata msimu huu ni kutokana na ubora wa wachezaji walionao. Na kikosi chake kilikuwa bora kwenye maeneo yote na ubora wao ni mkubwa ukilinganisha na wengine.
“Tulikuwa na msimu bora, tumefunga mabao mengi tumekuwa timu bora kwenye kushambulia timu bora kwenye ulinzi. Tumekuwa bora, nafikiri tumekuwa bora mbali sana kwa sababu tuna wachezaji bora, nataka niwapongeze wachezaji wote na sio Aziz peke yake.” amesema Miguel Gamondi
Young Africans imechukua ubingwa wa Ligi kuu kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Azam FC waliomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara msimu 2023-24. Yanga imemaliza ikiwa na alama 80, pia wameongoza kwa kufunga mabao 71 huku wakiruhusu mabao 14 tu ya kufungwa.