Mwana-Masumbwi mkongwe Mike Tyson (58), ameripotiwa kuugua juzi akiwa kwenye Ndege akitokea Miami kuelekea jijini Los Angeles.
Kwa mujibu wa msemaji wake, bingwa huyo wa zamani wa ndondi alianza kujisikia vibaya takribani dakika 30 kabla ya kutua.
Mara tu baada ya kutua alipokelewa na timu ya wauguzi na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
Mwaka 2022 picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilimuonyesha mkongwe huyo akiwa kwenye kiti cha magurudumu huku akiwa ameshikilia fimbo ya kutembelea katika maeneo ya Uwanja wa Ndege.
Baadaye Tyson aliweka wazi kuwa anasumbuliwa na mifupa na mishipa ya mgongo inayoleta maumivu hadi miguuni.
Tyson anatarajiwa kuchuana na mwanamitandao maarufu wa YouTube ambaye pia ni mwana ndondi Jake Paul (27) ifikapo Julai 20.