
๐ง๐ฎ๐๐ถ๐๐ผ ๐น๐ฎ ๐๐ถ๐บ๐ ๐ธ๐๐ท๐ถ๐๐ถ๐บ๐ฎ ๐๐ป๐ฎ๐ฝ๐ผ๐๐ฒ๐ธ๐ฎ ๐๐ถ๐ธ๐ถ๐ผ๐ป๐ถ ๐๐ต๐ถ๐ฑ๐ฎ ๐ก๐ถ๐ป๐ถ ??
Related Content
Related Content
Umeshawahi kuona simu yako unapoweka sikioni wakati umepigiwa au unasikiliza voice note inajizima ? Je shida inakuwaga Nini unakuta mtu kakupigia simu unaweka sikioni kioo kinazima.
Lazima ujue kwenye simu yako Kuna kitu kinaitwa ๐ฃ๐ฟ๐ผ๐ ๐ถ๐บ๐ถ๐๐ ๐ฆ๐ฒ๐ป๐๐ผ๐ฟ,ni ki hardware kidogo ambacho kinapatikana kwenye simu. Kimeundwa kwa kutumia electromagnetic utumika kupima umbali uliopo kati yako na kifaa unachomiliki.
Sababu kubwa ya kuwepo hii Proximity Sensor Kulinda maisha ya betri pale unapotumia simu.
Kulinda simu yako isijibonyeze bonyeze kwa bahati mbaya pale unapoweka karibu na sikio lako.
Mfano unapopiga simu au kupigiwa simu na mtu akapokea na kuweka sikioni basi Sensor ya proximity ufanya kazi ya kutambua simu yako umepigiwa hivyo inatoa ulinzi kwa kuweza kuzima simu yako na kioo kuwa (off) unapoweka kwenye sikio.
Hii inakusaidia kuhusu sikio au Uso wako (shavu) kujibonyeza bonyeza Sehemu ya kukata Simu au kujiandika andika pale unapoongea na simu au ukiwa umelala.
Pia utumika kufanya auto brightness kwenye simu yako kwa kuweza kukupunguzia mwanga au kuongeza unapoweka simu yako karibu na sikio au usoni.
Inafanya kazi kuanzia android version 8 na kuendelea FANYA HIVI ingia setting kwenye simu yako >> Display>> Tafuta Ambient display au lock screen display >> prevent accidental touch utaamua kuweka On au Off.
.