Anafahamika kama Thomas Fuller, Mtaalamu wa Hisabati wa Kiafrika anayejulikana pia kama “Negro Tom” na “Virginia Calculator”, alikuwa Mwafrika mtumwa aliyezaliwa Benin mwaka 1710 akijipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake wa kukukotoa hesabu, mpaka akitwa jina jingine pia la kikokotoo cha akili.
Fuller alisafirishwa hadi Amerika kama mtumwa mwaka wa 1724. Kiukweli Fuller alikuwa na uwezo wa ajabu wa kufanya hesabu, akigunduliwa kipaji chake na Wanaharakati wa kupinga utumwa ambao walimtumia kama maonesho kudhihirisha kuwa watu weusi walikuwa bora na si duni kuliko wazungu kitaaluma.
Taarifa zake zilienea kwa haraka na wakajitokeza watu ambao hupenda kuhakikisha mambo (Hartshorne na Coates), ili kujaribiu uwezo wake wakamuuliza kuna Sekunde ngapi ndani ya mwaka mmoja na nusu, na ilimchukua dakika mbili pekee kuwapa jibu lao kwamba zipo Sekunde 47,304,000.
Hawakutosheka, kwani walimpa tena swali la pili wakimuuliza ni sekunde ngapi mtu mwenye miaka 70, siku kumi na saba na saa kumi na mbili atakuwa ameishi? kwa umakini ndani ya dakika moja na sekunde 30 aliwajibu kuwa mtu huyo angekuwa ameishi kwa Sekunde 2,210,500,800.
Kisha likafuata swali la tatu, wakimuuliza kuwa “tuseme mkulima ana nguruwe sita, na kila nguruwe ana nguruwe sita, mwaka wa kwanza, na wote wanaongezeka kwa uwiano sawa, hadi mwisho wa miaka minane, mkulima atapata nguruwe ngapi na katika dakika kumi,” Fuller aliwajibu kwamba ni Nguruwe 34,588,806.
Safari hii alichelewa kidogo kutoa jibu, kwani tofauti ya muda kati ya kujibu kwake swali hili na maswali mawili ya awali, iliisababishwa na kosa dogo alilofanya kutokana na kutoelewa kwa ufasaha swali hilo, hivyo Hartshorne na Coates wakathibitisha kuwa uwezo wa Fuller kiakili ni mkubwa na lazima utakuwa mkubwa zaidi.
Katika maisha ya kawaida, Fuller akiwa Mtumwa alifanya kazi kwa bidii katika mashamba kwa maisha yake yote akizungumza kwa heshima na kwa umakini mkubwa akimtunza ya bibi yake ambaye anasema hakuwa tayari kumuuza, licha ya kuahidiwa kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa watu kadhaa waliokuwa wakinunua watumwa.
Mmoja wa waliokuwa wakimdadisi (Coates), baada ya kujiridhisha hali halisi ya uwezo wa kiakili wa Fuller alisema mbele yake kwamba, “inasikitisha huna elimu sawa na fikra zako,” lakini Fuller kwa furaha alimjibu akisema, “hapana, ni bora sikuwa na elimu, kwa maana watu wengi wasomi ni wapumbavu wakubwa.”
Ama kweli, akili ni nywele kila mtu ana zake. wakati msomi akisikitika kumuona Fuller hana elimu, yeye anaona wasomi ni wapumbavu, je? ni kwanini Fuller almaarufu kama ‘Kikokotoo’ anaona kwamba wasomi wengi wana shida? hili ni fumbo kwani hakuhojiwa ili kutoa sababu zake hivyo nikukaribishe kwa maoni utupatie mtazamo wako.