Siku ya jana Mei 29 2024, Afrika ya Kusini ilianza rasmi uchaguzi wake mkuu ikiwa huu utakuwa uchaguzi wa mara ya 8 kama hatua muhimu katika historia ya nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kikoloni mnamo Mwaka 1994.

0

0:00

Uchaguzi wa mwaka huu unaonekana kuwa na ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, huku kura za maoni zikionyesha kuwa chama tawala cha African National Congress ANC kinaweza kupoteza nafasi yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 madarakani.

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi yametangazwa (ANC) inaoonekana kuwa wenye ushindani zaidi nchini Afrika Kusini, ambapo tangu chama cha African National Congress (ANC) kiingie madarakani miaka 30 iliyopita hakikuwahi kupata mpinzani.

Huku matokeo yakionyesha kwa zaidi ya asilimia 11 ya wilaya za wapiga kura yamehesabiwa kufikia sasa, ANC inaongoza kwa 43%, ikifuatiwa na DA yenye 26%.

Ambapo Chama chenye msimamo mkali cha EFF na Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani Jacob Zuma vikiwa vina karibu 8%.

Si hivyo tu Kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30.

Hii ni kutokana na kupoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira.

Lakini ni mapema sana kutabiri matokeo ya mwisho. Uchaguzi wa Alhamisi ulishuhudia misururu mirefu ya wapiga kura nje ya vituo vya kupigia kura hadi usiku wa manane kote nchini.

Hata hivyo matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa juma hili.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading