Uongozi wa Arsenal una mpango wa kumsainisha mkataba mpya Kocha Mkuu wa Mikel Arteta, ili kuongeza chachu ya kumsajili na kisha kumsajili Mshambuliaji kutoka Slovenia na Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani Benjamin Sesko.

0:00

4 / 100

Gazeti la The Mirror limeripoti kuwa, hatua ya Arteta kutarajiwa kusaini mkataba mpya, itatumika kama silaha ya kumvuta Mshambuliaji huyo mwenye umri wa 20, ambaye kwa sasa anaongoza katika orodha ya wanaopigiwa upatu wa kusajiliwa huko Emirates Stadium.

Gazeti hilo limeandika: “Mikel Arteta yuko katika hatua nzuri kukamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya, kufuatia mazungumzo kati yake na Uongozi wa Arsenal kwenda vizuri.

“Mkataba wa sasa wa Kocha huyo kutoka nchini Hispania umebakisha mwaka mmoja, huku akijidhihirisha kuwa mmoja wa makocha wanaochipukia Barani Ulaya.

“Kwa sasa Arsenal wako sokoni kutafuta Mshambuliaji mpya huku Benjamin Sesko wa RB Leipzig akiongoza kwenye orodha iliyowasilishwa mezani kwa viongozi klabuni hapo.”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Russell fastest ahead of Las Vegas Grand...
LAS VEGAS, - George Russell topped the time sheets in...
Read more
ELON MUSK NDIYE MTU TAJIRI ZAIDI DUNIANI...
Dar es salaam Jarida linaloangazia masuala ya fedha ...
Read more
SABABU ZA BAKARI MWAMUNYETO KUGOMEA KURUDI YANGA
NYOTA WETU Nahodha wa timu ya Yanga amegoma kurejea kambini...
Read more
Brighton's Welbeck completes comeback win over Tottenham
Brighton & Hove Albion staged a storming second-half comeback with...
Read more
Erik Ten Hag atoa maoni yake juu...
MICHEZO Kocha wa Klabu ya Manchester United, Erik Ten Hag...
Read more
See also  Nathan Ake is taken off on a Stretcher in tears after horror Injury

Leave a Reply