WIMBI LA JOTO KALI INDIA LAUA WATU
Mji Mkuu wa India New Delhi, unakabiliwa na wimbi la joto kali hali iliyovunja rekodi hadi kufikia nyuzijoto 52.3C ( 126.1F).
Joto hilo limekuwa likisababisha Wanafunzi Mashariki mwa nchi hiyo kupoteza fahamu na watu kadhaa kupoteza maisha katika jimbo la Rajasthan.
Kwa mujibu wa muuguzi mmoja, joto hilo limesababisha miili ya wengi kuishiwa maji hivyo kupelekea hali za kuzimia, kutapika na kujisikia kizunguzungu.
India pamoja na sehemu za Asia ya Kusini na Asia ya Kusini Mashariki zimekuwa zikikabiliwa na joto kali tangu mwezi uliopita.
Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa hali hiyo itaanza kupoa kuanzia Alhamisi.
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.