Chama cha Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani, Jacob Zuma kimepata karibu asilimia 11 ya kura na chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kina asilimia 10.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kuwa hadharani mwishoni mwa wiki. Kwa mwendo huo, ANC italazimika kuungana na vyama vingine kwenye ubunge.
Wapiga kura wengi wanalaumu ANC kwa kusababisha uwepo wa kiwango cha juu cha vitendo vya ufisadi, uhalifu na ukosefu wa ajira nchini.
Baraza linaloheshimika la Utafiti wa Sayansi na Viwanda (CSIR) na tovuti ya News24 zimekadiria kuwa kura za mwisho za chama hicho zitakuwa karibu asilimia 42. Katika uchaguzi uliopita mwaka 2019, ANC ilipata asilimia 57 ya kura.
Haijulikani ikiwa Rais Cyril Ramaphosa atasalia madarakani, kwani anaweza kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa ANC kujiuzulu ikiwa chama kitapata chini ya asilimia 45.