FAIDA ZA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

0

0:00

Kujamiana (ama tendo la ndoa)ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu.Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhiahana katika tendo la ndoa.

Si hivyo tu,bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule.Je! Kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndio! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KIAFYA AMBAZO UTAZIPTA KAMA UTAKUWA UNASHIRIKI TENDO LA NDOA MARA KWA MARA MAISHANI MWAKO

1) Hupunguza msongo wa mawazo

Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono.
Kufika kileleni ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika na misuli kurelax).na hii ndio sababu kuu ya kwanini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana.

2) Hupunguza maumivu.

Kufika kileleni (orgasm) Wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu.Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa mgongo,kipandauso na kumfanya mtu kuwa na furaha isiyo na kikomo.

3)Huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini.

Unapojamiana na kufika kileleni, mzunguko wa damu huongezeka maradufu,hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.

4) Huongeza hali ya kujithamini.

Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na yakuvutia,haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na yakuvutia,hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yeyote.

See also  TUNDU LISSU AHOFIA USALAMA WAKE ATOA AHADI YA KUWATAJA WANAOMFATILIA

5) Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba.

Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wa kutunga mimba.Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanaume,huzifanya kuwa katika kiwango kizuri,na kama unataka kupata mtoto ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara itakusave sana.

6) Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume.

Wanaume walio na umri wa miaka 40 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wanauwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana.

7)Husaidia kuishi kwa muda mrefu.

Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa week hurefusha maisha yako.kila unapofikia kilele,homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosteron) hutolewa kwa wingi sana.Ambayo huongeza kinga ya mwili,hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda),huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo,huiweka ngozi kuwa na afya bora na kupunguza msongo wa mawazo.kwa hiyo kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.

8) Huongeza upendo baina yenu.

Kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano,uaminifu,unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading