Mchezaji nyota wa Al Ahly Hussein El-Shahat amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya pauni 100,000 za Misri kwa kosa la kumpiga Mohamed Chibi wa Pyramids kwenye mchezo ambao Al Ahly alifungwa Mabao matatu kwa bila msimu uliopita.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Hussein El-Shahat alionekana kumpiga Vibao Chibi huku akidai kuwa raia huyo wa Morocco (Chibi) alimtukana yeye na familia yake.
Uamuzi wa mahakama ulikuwa kama ifuatavyo;
“Mahakama ya Makosa ya Jiji la Nasr inamuhukumu Hussein El-Shahat kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya EGP 100,000, na kufungiwa kwa muda wa miaka mitano kutojihusisha na Mchezo soka.”