Mkurugenzi wa michezo wa AaB, Ole Jan Kappmeier amesema kuwa Kelvin John ni mchezaji wa mafanikio ambaye anaamini anaweza kujiendeleza zaidi akiwa klabuni hapo.
Aidha Mchezaji Kelvin John kupitia mazungumzo yake na AaB alisema;- “Mara ya kwanza kabisa AaB ilipoonyesha nia, nilidhamiria kuja hapa, na kupitia mazungumzo yangu na klabu nilipata taswira nzuri juu ya klabu hii na inanifaa kabisa”
“Natumai kwamba kwa kasi yangu, bidii yangu naweza kusaidia timu wiki baada ya wiki na wakati huo huo.
Kelvin amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia AaB hadi mwaka 2028 na atavaa jezi nambari 27 kuanzia msimu ujao.
“It’s always with where you start”
“Genkies, Ninashukuru kwa muda tuliotumia pamoja, daima nitaweka uhusiano wetu na upendo moyoni mwangu pamoja na kumbukumbu na matukio ndani ya akili yangu.
Natamani ningetumia muda mwingi nanyi lakini hatima ina mipango zaidi.
Nawatakia kila la kheri kwa siku zijazo, Daima mtabaki moyoni mwangu,” ameandika Kelvin John kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.