Lapid ametoa pendekezo la kuiunga mkono serikali iwapo washirika wa serikali ya Netanyahu wataukataa mpango huo uliotangazwa na Biden.
Familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas wametaka pande zote mbili kuukubali mpango huo wa kumaliza vita vilivyodumu kwa miezi minane sasa na kutaka jamaa zao kurejea nyumbani, lakini Israel imeendelea kusema masharti ya kusitisha mapigano lazima yatimizwe kwanza.
Rais wa Marekani Joe Biden siku ya jana alieleza namna mpango huo wa hatua tatu wa kusitisha mapigano utakavyotekelezwa.
Hatua ya kwanza itakuwa ni kipindi cha wiki sita cha usitishaji mapigano ambacho kitashuhudia vikosi vya Israel vikiondoka kwenye miji yote iliyo na watu wengi kwenye Ukanda wa Gaza.
Kisha itafuatiwa hatua ya pili na ya tatu inayojumuisha kubadilishana mateka wote na wafungwa, na baadae vikosi vya Israel vitaondoka kikamilifu na mpango wa kuijenga upya Gaza utaanza..