Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea wameshuhudia utiaji saini wa mkataba mmoja, hati za makubaliano (MOU) 2 na tamko la pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi (EPA).

0:00

10 / 100

Mkataba huu utaiwezesha Tanzania kupokea mkopo kutoka Korea wa kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia (2024- 2028) kwa ajili ya miradi ya miundombinu ya maendeleo zinatolewa chini ya Mfuko wa
Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea (EDCF).

Ili kufungua milango zaidi ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi, Tanzania na Korea zimesaini pia mkataba wa EPA utakaowezesha kuufanya uhusiano kuwa wa kimkakati
hususan katika Nyanja za Biashara, Uwekezaji, Viwanda, Usafirishaji n.k.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi 3 tu barani Afrika ambazo zitafanya majadiliano hayo yatakayozaa Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Korea, Nchi nyingine ni Morocco na Kenya.

Hati za Makubaliano zilizotia saini leo ni pamoja na Ushirikiano katika Uchumi wa Buluu ambapo Tanzania itashirikiana na Korea Kusini katika maeneo ya uvuvi, viwanda vya kuchakata mazao ya bahari, ujenzi wa bandari za uvuvi, teknolojia na tafiti za masuala ya bahari, pia Wizara ya Madini ya Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Korea Kusini zimetia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Madini ya Kimkakati.

Tanzania na Korea Kusini zitashirikiana katika utafiti, uwekezaji, uchimbaji na kujenga uwezo wa kuongeza thamani ya madini ya kimkakati chini Tanzania. Madini hayo ni Nickel, Lithium na Kinywe.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DARAJA LA FRANCIS SCOTT KEY LAUA WATU...
HABARI KUU Sita wahofiwa kufa tukio la daraja kuporomoka Marekani Huku...
Read more
Chen Tang Jie-Toh Ee Wei have booked...
Mixed doubles pair Chen Tang Jie-Toh Ee Wei have booked...
Read more
SIMBA YAIPUMLIA YANGA ...
MAGAZETI
See also  WIVES WHO CAN'T HANDLE THE TRUTH
https://youtu.be/opRwA4-OsQk?si=mCOTeC2o5Y15MgRq Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
WHY FOREPLAY IS IMPORTANT FOR MARRIED COUPLES
LOVE ❤ Foreplay is the act of flirting, fondling, licking,...
Read more
Great Blue Heron working on its catch
Ac tortor dignissim convallis aenean et tortor at. Nisl...
Read more

Leave a Reply