PETER MSIGWA ASHTUKA KUCHEZEWA RAFU UCHAGUZI NDANI YA CHADEMA

0:00





Baada ya Siku chache kupita tangu Joseph Mbilinyi (Sugu) kutangazwa kuwa Mshindi wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa.

Mapema leo June 3, 2024 Aliyekuwa Mgombea wa Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ametangaza kukata rufaa ya kupinga matokeo hayo akidai kuwa Mchakato wa Uchaguzi huo haukuwa halali ikiwemo baadhi ya Wanachama Waliostahili kupiga kura kuzuiliwa kufanya hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari na Wanachama wa CHADEMA Manispaa ya Iringa, Msigwa amesema kuwa Uchaguzi huo haukufuata utaratibu wa Kikatiba wa Chama hicho huku akieleza kuwa kulikuwa na Mazingira yaliyoandaliwa kwa ajili ya Mpinzani wake kushinda.

“Msimamizi wa uchaguzi alifanya kampeni ya kuniondoa katika nafasi akidai kuwa yalikua ni maelekezo kutoka uongozi wa juu kwa hoja kuwa nimekaa madarakani kwa muda mrefu, kulikua na figisu ikiwa ni pamoja na kuvurugwa kwa chaguzi za baadhi ya mikoa ikiwemo Mkoa wa Njombe ambako nilikua na wafuasi wangu” amesema Msigwa

Msigwa ameongeza kuwa baada ya kukata rufaa hiyo ataendelea kusalia kwenye Chama hicho hata kama rufaa yake haitabadilisha Matokeo ya Ushindi wa Mpinzani wake.

“najua wabaya wangu wengi walikuwa wanatoa ramli labda mimi leo nitahama siondoki siendi popote nipo CHADEMA sihami CHADEMA tutapambana humu humu yule anayetaka kunyofowa wengine atanyofolewa yeye tunachotaka haki itendeke hatutoogopa cheo cha Mtu wala sura ya Mtu” ameongeza Msigwa

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WANAOUZA DAWA BILA BARUA YA DAKTARI WAONYWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
Davido went on his social media account...
“Anybody wey do me bad go collect this year one...
Read more
Zverev to face Humbert on return to...
Third seed Alexander Zverev produced a near-flawless display to outclass...
Read more
DON 3 KUACHILIWA BILA MKALI SHAHRUKH KHAN...
Nyota Wetu
See also  TLS Yaanika Wazi Orodha Ya Waliotekwa na Kupotezwa
Hii ni habari kama isiyopendeza kwa mashabiki wa nguli...
Read more
Late double saves Tottenham and ends Coventry's...
Brennan Johnson scored a stoppage-time winner as Tottenham Hotspur hit...
Read more

Leave a Reply