Licha ya msimu ujao Simba sc kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika, lakini wataanzia katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo, huku Yanga sc watakaocheza Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika nao wakianzia hatua hiyo.

0:00

9 / 100

Mashindano ya CAF msimu wa 2024/25 yataanza kwa raundi ya awali kati ya Agosti 16 hadi 18 Agosti, 2024 huku hatua za makundi zikipangwa Oktoba hadi mwezi Desemba mwaka 2024.

Klabu ya Yanga SC itaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye raundi ya pili michuano hiyo na wataanzia ugenini huku Simba Sc ikianzia raundi ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika nayo itaanzia ugenini.

Licha ya Azam FC kusiriki Klabu Bingwa, lakini wao wataanzia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Coastal Union wakianzia raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC na Coastal Union wataanzia nyumbani kwenye michuano hiyo. Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za Afrika zitakazoingiza timu nne kwenye mashindano ya CAF.

Nchi nyingine ni Algeria, Angola, Ivory Coast, Misri, Libya, Morocco, Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini, Sudan na Tunisia.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya awali utafanyika kati ya tarehe Julai 1, 2024 hadi Julai 20, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya pili utafanyika kati ya tarehe Julai 21 hadi Agosti 31, 2024.

Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya makundi utafanyika kati ya Septemba 1 hadi Septemba 30, 2024.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Frustrated PSG held to goalless draw at...
AUXERRE, France, 🇫🇷 - Ligue 1 leaders Paris St Germain...
Read more
TECHNIQUES OF CONFLICT RESOLUTION
LOVE TIPS ❤ 10 TECHNIQUES OF CONFLICT RESOLUTION THE SLEEP AND...
Read more
MASHABIKI WA AJAX WAFANYA VURUGU KISA MATOKEO...
Michezo Nchini Uholanzi hapo jumapili kwenye mchezo kati ya Ajax...
Read more
Chelsea star Enzo Fernandez has been banned...
The Argentine footballer had already been found guilty of failing...
Read more
NDEGE ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS YAPOTEA
HABARI KUU
See also  SEX TIPS FOR HUSBANDS
Ndege ya kijeshi iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais...
Read more

Leave a Reply