Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) imethibitisha kuwa msimu ujao utakuwa na Usaidizi wa Mwamuzi (VAR) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wa Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa TPLB Almas Kasongo amesema VAR itakuwepo katika uwanja huo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
“ Msimu ujao tutakuja tofauti kidogo. Tutaboresha na tuna mpango wa kuwa nayo na CAF ndiyo wametuunga mkono na baadhi ya wataalamu wameshafika na kufunga vifaa hivyo katika Uwanja wa Mkapa.
Kasongo aliongeza kuwa uwepo wa teknolojia hiyo itakuwa sehemu ya kuwasaidia waamuzi wa Tanzania.
“ Tunaamini safari moja huanzisha nyingine, tutakuwa na katika viwanja vingine kuna partnes wetu watasaidia kwa ajili ya viwanja vingine” alisema Kasongo.
Uwepo wa VAR utakuwa nafuu ya kupunguza lawama kwa waamuzi kwa timu za Simba SC na Yanga SC ambazo zimekuwa zikiweka shinikizo kwa waamuzi katika baadhi ya michezo yao.
Related Content