RC CHALAMILA AWAPA MAKAVU WASOMI WANAOLIA AJIRA ‘TWENDENI KARIAKOO MKAONE MAISHA YA WASIOSOMA

0:00

9 / 100

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka ‘wasomi’ wa vyuo vikuu kuacha kukata tamaa Kwa kigezo cha kukosa ajira, na kubaki na mtazamo wa kuilaumu Serikali Kwa kushindwa kuwapa ajira, jambo ambalo linawalemaza na kupelekea kukosa ubunifu wa kutafuta mbinu za kujiajiri.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Juni 03, 2024 katika ziara yake kwenye chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni – Kigamboni Jiji humo chenye zaidi ya wanafunzi 14,000, alipokwenda Kwa lengo la kukutana na kuzungumza na wanafunzi hao pamoja na watumishi, pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Maktaba itakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2,500 kwa wakati mmoja pamoja na ukumbi wa mihadhara ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu sio chini ya 1000.

“Usiwe Mkata tamaa, maisha hayapo hivyo na sio mepesi Kila wakati uyatafsiri Kwa mlengo wa kisiasa, nimekuja kuwatia moyo na kuwaondolea wasiwasi, ukiona watu kumi hawajaajiriwa nawewe unajiunga kwenye msafara unahoji ‘Sasa hii Elimu ya nini’? mkiona mmeelemewa kabisa na mnaanza kufikiria njooni niwakodie mabasi twende pale Kariakoo tuwahoji ambao hawajaingia darasa hata moja wamejaribu kwa namna kubwa kufanikiwa, wewe unalalamikia mtaala, achana na mitaala, twende Kariakoo ambapo mtaala hawaujui, amesema RC Chalamila.

Aidha, RC Chalamila amepokea kero mbalimbali ambazo wanafunzi wa chuo hicho hukabiliana nazo ikiwemo kupokea kiasi cha pesa cha mkopo pungufu na ilivyo katika makubaliano ambapo ameiagiza bodi ya mikopo kufanyia kazi Changamoto hiyo na apatiwa mrejesho.

Sanjari na hilo RC Chalamila ameahidi kufanyia kazi Changamoto zote alizoelezwa ikiwemo kuonana na Waziri mwenye dhamana ya elimu ili kupata Suluhu za Changamoto hizo.

See also  Mpango amwakilisha Rais Samia Kwenye Mazishi ya Saulos Chilima

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Prof Shadrack Mwakalila amesema chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Pamoja na kutoa fani mbalimbali bado kimeendelea kujikita katika fani za uongozi na maadili na utawala hivyo wanafunzi wanaopita katika chuo hicho wameandaliwa vizuri katika nyanja ya uongozi, maadili na utawala.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SIMBU ASHINDA TUZO CHINA
NYOTA WETU. Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Simbu ameshika nafasi ya...
Read more
12 WRONG THINGS GIRLS CHECK BEFORE MARRYING...
LOVE ❤ Many Ladies are known to base their marital...
Read more
'Real Reason I started smoking’ – Rema
Afrobeats star Divine Ikubor, popularly known as Rema, has opened...
Read more
DAVIDO LAUNCHES NEW COURSE AT UNIVERSITY OF...
OUR STAR 🌟 Nigerian singer and songwriter David Adedeji Adeleke,...
Read more
Hall of Fame designated hitter Edgar Martinez...
New Seattle skipper Dan Wilson announced the hire on Friday,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply