Awali kiungo huyo raia wa Burkina Faso alichapisha taarifa ya kuushukuru uongozi wa klabu hiyo, mashabiki pamoja za wachezaji wenzie kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu uliomalizika hali iliyopelekea wengi kudhani anaaga Yanga.
Hata hivyo Aziz Ki amejibu ‘comment’ ya mdau iliyosema “Ashiiii Azizi sasa kwenye post yako usianze na maneno ‘thanks’ unatufanye tuhofie kuwa unataka kuondoka”
Akijibu ‘comment’ hiyo Ki ameandika “Nawashukuru kwa sababu ni jambo dogo sana ninaloweza kufanya kuwashukuru nyinyi ambao mnanisaidia kila siku, SIO KWAHERI NIKO HAPA MSIJALI”
Posti iliyozua sintofahamu ilisomeka “Kila kitu kiliwezekana Shukrani kwenu wachezaji wenzangu, wafanyakazi, kamati ya rais na hasa nyinyi mashabiki, wapendwa wangu, familia na pia kwa baraka za Mungu mwema
kwa mara nyingine tena asante kwa uaminifu wako, msaada wako, imani yako, umenipa mengi katika msimu wote”