Amethyst ni moja kati ya vito vya thamani vinavyojulikana kama SEMI PRECIOUS GEMSTONES vikitanguliwa na Ruby (Marijani), Diamond (Almasi), Emerald (Zumaridi) na Sapphire (Yakuti Samawi) ambavyo hujulikana kama VERY PRECIOUS GEMSTONES.
Amethyst ni jiwe la zambarau lenye mvuto wa aina yake.
Limeundwa kwa madini ya Silicon, Oxygen na chembe chembe za madini ya Chuma (Iron crystals)
Watu mashuhuri wa zamani walipenda sana kutumia jiwe hili kama pete, mikufu au bangili (bracelet)
Watu mashuhuri wa zamani kama vile Malkia Cleopatra wa Misri, Malkia Mary wa Uingereza na Leonardo da Vinci wa Italia, walipenda sana kuvaaa Pete zilizotengenezwa kwa Kito cha Amethyst.
✍️Amethyst ni jiwe la kiroho linalochochea kufunguka kwa jicho la tatu (third eye) kwa urahisi na kufungua crown chakra.
✍️Amethyst hutumiwa na watu wanaotaka kuamka kiroho kupitia Tahajudi (meditation) kwa sababu ni jiwe linaloamsha consciousness kwa urahisi wakati wa kufanya tahajudi.
✍️Unapokuwa ukifanya meditation, weka jiwe lako kwenye paji la uso ukiwa umelala chali, utaingia kwenye urazini kwa urahisi na kufungua jicho la tatu bila kusumbuka.
Au unaweza kushika jiwe lako kwenye mkono wako wa kushoto wakati ukifanya tahajudi ili kukusaidia kudhibiti mawazo yasiendelee kuzunguka zunguka huku na kule.
✍️Amethyst hutumiwa na watu wa nyota ya Punda (Aries) kudhibiti maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.
✍️Huchochea hali ya utulivu wa akili na kusababisha usingizi mtamu (sweet sleep)
✍️Aidha, jiwe la Amethyst, hutumiwa na watu wengi kudhibiti nishati hasi na kuondoa aina zote za nguvu hizo ndani ya siku 90.
Wachina hulitumia jiwe hili kujikinga na uchawi wa kila aina.
✍️Amethyst inasaidia kuboresha mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kudhibiti magonjwa ya kila aina yasiweze kushambulia mwili wa binadamu kwa urahisi.
✍️Jiwe hili, likitumiwa pamoja na jiwe la Citrine huchochea kipato kukua na kuongezeka.
✍️Jiwe la Amethyst limedhibitika kudhibiti ulevi.
Kwa ujumla hili ni jiwe lenye faida nyingi za kiroho, kisaikolojia na kimwili pia.
Unaweza kutumia jiwe la Amethyst likiwa kwenye Pete, Mkufu, Bracelet, Hereni nk; lakini hupendeza zaidi likivaliwa kama Pete.
Jiwe hili ni maalum kwa watu wa nyota za Ndoo na Samaki waliozaliwa mwezi February, lakini vile watu wote (nyota zote) wanaweza kutumia jiwe hili na kunufaika na faida zake.
