SERIKALI YAJA NA MWAROBAINI KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU MIPAKANI

0:00

HABARI KUU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, ametoa mwezi mmoja kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuhakikisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mipaka unafanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji Manyovu ili kuepusha upotevu wa mapato ya nchi, kuepusha mifumo ya rushwa na kudhibiti uingiaji wa watu wanaoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shughuli za uingiaji na utokaji wa raia na wageni wanaokwenda nchini Burundi kupitia Kituo cha Uhamiaji Manyovu kilichopo katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo pia amewataka kuhakikisha wanadhibiti vipenyo mbalimbali vinavyopatikana katika mpaka huo.

‘Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama na hilo ameshalitekeleza na mtaona jinsi alivyowapandisha vyeo askari wa ngazi mbalimbali lakini sasa wajibu uenda sambamba na haki kwahiyo lazima muongeze jitihada katika kufanya kazi zenu,haiwezekani Waziri ndio aje hapa kufuatilia suala la mfumo,mara sijui mfumo wa kiyoyozi haufanyi kazi, sasa nishamuelekeza Kamishna Jenerali kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mfumo huo unafanya kazi,haiwezekani serikali imewekeza fedha nyingi katika mfumo huu wa uhamiaji mtandao sasa haiwezekani leo usiwe unafanya kazi mnakaa kubeba fedha za wananchi na kuzipeleka benki kwa njia ya kawaida” alisema Waziri Masauni.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mfawidhi wa Kituo cha Manyovu, Inspekta Arnold Masha aliweka wazi hali ya uingiaji na utokaji wa wageni kupitia kituo hicho ambapo jumla ya wageni na raia wa Tanzania 38,624 waliingia na kutoka nchini kupitia mpaka wa Manyovu na jumla ya wakimbizi raia wa Burundi 3,667 walipita katika mpaka huo wakirejea nchini kwao kwa hiari tangu Machi mpaka Mei 2024 huku Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kanali Michael Nhayalina akiahidi kuimarisha utendaji na kuyafanyia kazi maagizo ya serikali yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni.

See also  SERIKALI YA NIGERIA YAFANIKIWA KUWARUDISHA MATEKA 137

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

RASHFORD APIGWA NA MPENZI WAKE HOTELINI
NYOTA WETU Marcus Rashford wa Manchester United alizozana na mpenzi...
Read more
NESI ASIMULIA JINSI WALIVYOMPOKEA TUNDU LISSU ALIPOPIGWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
TFF YAPIGWA FAINI NA CAF ...
MICHEZO Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imetozwa kiasi...
Read more
MJAMZITO WA MAPACHA WA MIEZI NANE ACHINJWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
"KUNA MCHEZO MCHAFU WA KODI" SAMIA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply