OMchezaji wa timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Al Nassr, Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wanaomiliki magari ya kifahari na bei ghali zaidi duniani. Miongoni mwa magari yake ni pamoja na Bugatti Chiron, Lamborghini Aventador, Rolls-Royce Cullinan, Buggati la Voiture Noire na Buggati Veyron Grand Sports Vitesse.
Lionel Messi, mchezaji kutoka Argentina na Inter Miami pia anamiliki mkusanyiko wa magari ya kifahari na ya bei ghali zaidi ambapo baadhi ya magari yake ni Ferrari 335 S Spider Scaglietti, Maserati GranTurismo MC Stradale, na Audi R8.
Wachezaji wengine wa mpira wa miguu wanaomiliki magari ya bei ghali ni pamoja na Son Heung – Min anayemiliki Ferrari Laferrari, John Terry akimiliki Ferrari 275 GTB, Samuel Eto’o naye akimililki gari aina ya Aston Martin one -77.
Karim Benzema anamiliki Buggati Veyron 16/4 PUR SANG na mchezaji mwingine ni Zlatan Ibrahimovic yeye anamiliki gari aina ya Ferrari Monza SP2.