Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamemteua Mhe.Veronica Mueni Nduva kutoka Jamhuri ya Kenya kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

0

0:00

Mabadiliko hayo katika Sekretarieti ya EAC yamefanyika baada kuondolewa kwa Peter Mathuki Machi 8, ambaye anashutumiwa katika mambo mbali mbali hasa matumizi mabaya ya madaraka.

Rais Ruto alimwita Mathuki nyumbani na kumteua kuwa Balozi wa Kenya nchini Urusi.

Mkutano huo umefanyika wakati ukanda wa Afrika Mashariki ukikabiliwa na uhaba mkubwa wa pesa.

Mwezi uliopita, Mahakama ya haki ya Afrika Mashariki (EACJ) ilitangaza kusitisha shughuli zake mwezi Juni mwaka huu baada ya kukumbwa na matatizo ya kifedha yaliyotokana na ucheleweshwaji wa kutuma pesa kutoka kwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Veronica Nduva raia wa Kenya, ameapishwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuchukua nafasi ya Peter Mathuki aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo miezi kadhaa iliyopita, baada ya kuteuliwa na rais wa Kenya William Ruto kuwa Balozi nchini Urusi.

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya Mwenyekiti wake rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, wamekutana jioni hii kwa mfumo wa video, kushuhudia upiapisho huo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  KATUMBI KUWANIA URAIS DRC
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading