Mwanasiasa mkongwe Narendra Modi (73), leo amekula kiapo mbele ya Rais Draupadi Murmu wa India kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu katika sherehe kubwa iliyofanyika Ikulu.
Katika sherehe hiyo Mawaziri wa Baraza jipya nao waliapishwa. Jiji la Delhi lilikuwa na ulinzi mkali, huku Ikulu ikizungukwa na zaidi ya askari Polisi 2,500, na hakuna Ndege iliyoruhusiwa kuruka ama kupita.
Modi ameahidi kuongoza kwa haki bila upendeleo wala ubaguzi, na amesema kuwa kipaumbele chao ni kuwawezesha masikini na watu wa tabaka la kati.
Maelfu ya wageni walihudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi kutokea nchi za jirani kama Bangladesh, Nepal,Sri Lanka na Maldives.