WANAUME WENYE MALENGO YA KUOA WANA UMRI HUU NA WANA SIFA ZIFUATAZO

0:00

MAPENZI

DADA YANGU KABLA HUJAANZISHA MAHUSIANO NA MWANAUME HUU NDIO MGAWANYO WA WANAUME KULINGANA UMRI WAO

  1. WANAUME wenye miaka 20-27 wengi hawana nia na ndoa au mahusiano yenye kesho labda wale wa vijijini. Kijijini vijana wengi huoa kwasababu kama waongeze nguvu kazi ya familia, mahari mara nyingi zinatoka kwa wazazi sio zao (hawajazitesekea) lakini wanaume waliko mjini kwa 20-27 wengi ni wanafunzi na wanakimbizana na ndoto zao huwa si rahisi kuingia kwenye ndoa. Kwahiyo, ukianzisha naye mahusiano ni vigumu sana kukuoa kwasababu ana kiu na hofu ya MAISHA sana. Wanaume walioko kijijini mara nyingi hawayatazami maisha nje ya kulima na kuvuna zaidi wao wanatafuta kwa ajili ya muda uliopo si kwa ajili ya hatma zao njema. Kwahiyo dada yangu mwanaume akiwa chini ya miaka 28 akiwa mjini ukianzisha mahusiano ni vigumu kuwaza ndoa kwake.
  2. WANAUME WA UMRI WA MIAKA 28-31 hawa huwa wameshapevuka na wameanza mipango ya maisha anaweza akawa hana mafanikio ila angalau au ameshaona wapi anahitajika kufanya nini na utoto huwa umepungua zaidi labda awe hana dira yaani awe bado mgalatia au ameamua kuishi maisha ya KIGALATIA. Wengi wa 28-31 huwa si wanafunzi tena wamemaliza masomo wanajitafuta mtaani, wamepata pakushika, wanajimudu kwenye mambo yao muhimu na wanawaza kuanzisha mahusiano ya kudumu ili wasogee mbele. Wengi huwa hawajajipata sana ila huhitaji mahusiano yenye malengo. Hawa watu huonekana wakorofi sana kwasababu wana uchungu na mafanikio hasa mwanamke akija kwenye maisha yake anataka bata.

Hapa ndipo wanawake wengi huachwa wakionekana wanashindwa kuwa kwenye malengo, hapa ndipo single father wengi hupatikana kwasababu vijana wengi huanza kuishi na wanawake kabisa kama wake au hujiachia kwenye mahusiano yao wakiamini hao ndio watakuwa wake zao. Maisha ya wanaume hao yakiyumba wanawake huwakimbia hao vijana wakiwa tayari wamezaa nao au wanawake wakitaka maisha nje ya uhalisia huachwa nao vijana kwasababu wao wanawaza kusimama kiuchumi huku wanawake hao wakihitaji maisha nje ya uhalisia.

  1. WANAUME wa umri wa 32-38 hawa ni wanaume waliopitia mengi kupoteza, kuumizwa na kuumiza pia. Hawa huwa na mambo mawili kumpata mwanamke wa rika lake au linaloendana na lake hawapendi vidada kwasababu wengi huwa wameumizwa sana na wadada wadangaji. Hawa wao hutafuta mwanamke aliyemaliza ujana kama yeye na anayeyajua maisha na aliyevuka hatua za UGALATIA.
  2. WANAUME wenye miaka 40 na kuendelea hawa wao hutafuta mwanamke anayeweza kumheshimisha kuwa na ndoa au familia baada ya kupigiwa kelele kwa nini haoi, kuchezea ujana sana, watoto aliozaa nje akitaka apate mtu wa kuwalea yaani awakusanye.
See also  MADHARA YA FANGASI UKENI NA TIBA YAKE

Hapa kuna makundi mengi Kama

  1. Waliochelewa kuoa kwasababu ya utafutaji usio koma au kusoma sana mpaka muda wa kuwa na familia ukataka kuwapa kisogo watu hawa wengi huwa wana changamoto zao kwasababu hawana uzoefu wa mahusiano wao hutaka mahusiano ya haraka sana na kuoana na kuzaa haraka kukimbiza na umri. Mwanamke akichelewa kumzalia huhaha sana na anaweza kuzaa nje.
  2. Kundi jingine ni wale wanaokimbia ndoa zao baada ya kuvumilia sana wakaachika ili waoe tena waishi kwa amani hawa huwa walishakuwa kwenye ndoa tayari na wakazikimbia
  3. Kundi jingine ni wale wanaotaka kuongeza wake kwa matakwa yao baada ya kuona wamejipata kwenye maisha ya kuoana wanahitaji kwasababu wamepata uzoefu wa ndoa nk. Kwahiyo huanzisha mahusiano na ndoa ya pili au zaidi
  4. Kundi jingine ni wale waliofeli maisha wanatafuta kulelewa wanatelekeza ndoa au mahusiano yao ya awali ili wakalelewe.

WANAUME wa umri huu hutafuta single mother, vibinti vidogo wanavyoweza kuvilea muhimu viwazalie watoto hasa ambao wanatoka kwenye familia duni au wanawake wenye uhitaji na ndoa ambao hawachagui mume

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

BOT NA WACHUMI WA FEDHA WATOFAUTIANA WAKATI...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
HOW TO CALM YOUR HUSBAND'S MIND…
MAKE LOVE TO HIMSe* has a way of relaxing a...
Read more
UKOSEFU NA UHABA WA SUKARI NA UMEME...
HABARI KUU Serikali ya Tanzania imesema hadi kufikia mwezi Machi...
Read more
WHAT INSPIRES FAITHFULNESS IN MARRIAGE ...
LOVE ❤ 1. VISIONVision gives one a reason to stay...
Read more
3 THINGS YOU CAN DO TO INCREASE...
The strategies we apply for daily sales isn't rocket science.Truth...
Read more

Leave a Reply