AFYA
Kumekuwa na imani nyingi kuhusu dalili za mimba ya mtoto wa kiume katika mimba Changa na kina mama wengi wajawazito wanakuwa na shauku kubwa kujua jinsia za watoto wao waliopo tumboni mapema kabla ya kujifungua.
Mojawapo ya imani hizo ni kama;
- Mimba ya kiume huwepo endapo Mama mjamzito akiwa na dalili za kutapika au kichefu chefu asubuhi kidogo na kinyume chake huwa ni mtoto wa kike.
- Tumbo la mama mjamzito mwenye mtoto wa kiume tumboni huwa chini zaidi na hii kinyume na mtoto wa kike ambapo tumbo huwa juu karibia na kifua cha mama.
- Mama mjamzito mwenye mtoto wa kiume tumboni mabadiliko ya mood huwa ni kidogo kuliko yule mwenye mtoto wa kike ambapo huwa ana mabadiliko ya mood zaidi.
4.Mama mwenye mtoto wa kiume tumboni hupendelea kula vyakula vichungu kama ukwaju,Ndimu mbichi na Nyanya chungu tofauti na mama mjamzito mwenye mtoto wa kike tumboni ambaye hula vitu vitamu.
- Mama mjamzito mwenye mtoto wa kiume huwa mzuri katika ngozi yake zaidi kuliko wa kike ambaye huwa na chunusi na madoa madoa usoni.
6.Mama mwenye mtoto wa kiume tumboni mapigo ya Moyo ya mtoto huwa chini ya 140Bpm ukilinganisha na yule wa kike ambapo huwa juu ya 140Bpm.
✅UKWELI WA KISAYANSI✅
❤️Unataka kujua jinsia ya mwanao hakikisha ukifikisha wiki 20 kwenda juu(miezi 5) yaa ujauzito, uende hospitali na ufanyiwe ultrasound hiyo itakuonesha jinsia ya mtoto wako 99%-100%.