0:00
Ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Claus Chilima pamoja na watu wengine 9 imepotea asubuhi ya leo nchini Malawi.
Ofisi ya Rais imethibitisha kuwa Dr.Chilima alikuwemo kwenye ndege hiyo. Wengine ni pamoja na mke wa Makamu wa Rais Bi.Mary Chilima na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bi.Patricia Shanil Dzimbiri.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameahirisha safari yake ya Bahamas na ameamuru mamlaka zote husika kuungana katika kuitafuta Ndege hiyo.
Hadi taarifa hii ilipofika kwenye vyombo vya habari mchana wa leo, juhudi zote za mawasiliano na ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Lilongwe kuelekea Mzuzu zilikuwa zimefeli.
Related Posts 📫
HABARI KUU
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amefungiwa kuhudhuria vikao...
MANCHESTER, England 🏴 — Mason Mount was consoled by his...
Factbox on Dutchman Erik ten Hag, who was sacked as...
NYOTA WETU
Mwaka 2020 kijana Ilerioluwa Oladinaji Aloba alijiunga na Marlian...