HUNTER BIDEN AKUTWA NA HATIA YA MASHTAKA MATATU

0:00

9 / 100

Hunter Biden (54), ambaye ni mtoto wa Rais wa Marekani Joe Biden, amekutwa na hatia katika Mashtaka yote matatu ya uhalifu yaliyokuwa yakimkabili.

Jopo la waamuzi 12 wamemkuta Hunter na kosa la kulaghai kuhusu matumizi ya dawa za kulevya wakati alipokuwa akinunua bunduki mwaka 2018.

Makosa mengine ni kutoa taarifa za ulaghai kwa muuzaji wa silaha na kumiliki silaha akiwa ni mraibu wa dawa za kulevya kinyume na sheria.

Hukumu ya kesi hii inaweza kuwa kifungo cha hadi miaka 25, hata hivyo hukumu kubwa na ndefu kiasi hiki hutolewa kwa nadra kwa mkosaji wa mara ya kwanza.

Hunter anakuwa mtoto wa kwanza wa Rais wa Marekani aliye madarakani kukutwa na hatia ya uhalifu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Rais Vladimir Putin hawezi Kupigwa Risasi...
Kwanini Kilichomfika Trump Ni Vigumu Pia Kumfika Vladimir Putin..? Jibu: Wiki moja...
Read more
18 WAYS TO FIX YOUR WIFE IN...
LOVE TIPS ❤ 19 WAYS TO FIX YOUR WIFE -...
Read more
SIMBA YAFUNGULIWA KUSAJILI
MICHEZO Shirikisho la mpira wa miguu ( FIFA ) limeiondolea...
Read more
Konate injury clouds Liverpool's horizon ahead of...
Liverpool are sweating on the fitness of central defender Ibrahima...
Read more
A DIFFERENCE BETWEEN A COMPANY PROFILE &...
BUSINESS PLAN A business plan is a written document that outlines...
Read more
See also  Tips To Help Your Chickens Lay More Eggs

Leave a Reply