Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda.
Kufuatia hatua hiyo, amemteua Kenan Kihongosi kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi huo Kihongosi alikuwa mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Bw. Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba na anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais Dkt. Samia amemteua Bw. Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Kabla ya uteuzi, Bw. Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.
Aidha Dkt Samia amemteua Bw. Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Bw. Magala anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Vilevile Dkt. Samia amemteua Bw. George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Bw. Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.