AJALI YA BOTI YAUA WATU 80

0:00

Watu 80 wamefariki dunia baada ya Boti kuzama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rais wa nchi hiyo amethibitisha Felix Tshisekedi.

Maafa hayo yalitokea jana Jumatano kwenye Mto, Kilomita 70 kutoka Mji wa Mushie katika Jimbo la Maï-Ndombe karibu na mpaka wa nchi jirani ya Congo-Brazzaville.

Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Rais Félix Tshisekedi alisema amehuzunishwa na kifo cha raia wake.

Rais huyo alisema walioathiriwa watapata usaidizi na pia akaagiza uchunguzi ufanyike kubaini kilichosababisha maafa hayo.

” Rais wa Jamhuri ya Congo anatoa wito wa uchunguzi kuhusu sababu za kweli za tukio hili la kusikitisha, ili kuzuia maafa kama haya yasijitokeze tena katika siku zijazo,” ofisi ya rais ilisema kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.

Ajali mbaya za boti ni za kawaida nchini DR Congo, ambapo boti mara nyingi hujaa abiria ambao ni nadra kupewa jaketi za usalama na mara nyingi hawawezi kuogelea.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TIWA SAVAGE REVEALS SHE BECAME AN ARTIST...
CELEBRITIES Nigerian vocalist Tiwa Savage has revealed that she became...
Read more
PALESTINA SASA RASMI AMETAMBULIKA KAMA NCHI HURU
HABARI KUU Habari kubwa siku ya leo ni kuwa Baraza...
Read more
Lacklustre PSG concede home draw against PSV
PARIS, - Paris St Germain's weaknesses on the biggest stage...
Read more
Glasgow confirmed as the hosts of the...
Glasgow was confirmed as host of the 2026 Commonwealth Games...
Read more
UNDERSTANDING VIRGINITY, HYMEN, BLEEDING AND FIRST TIME...
LOVE TIPS ❤ Ladies keep getting confused in these areas...
Read more
See also  Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Mjane wa Reginald Mengi

Leave a Reply