AJALI YA LORI NA COASTER YAUA WANNE NA KUJERUHI WANNE MUHEZA

0:00

10 / 100

Watu wanne wamefariki Dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika Ajali ya Lori la mizigo ( T 925 CAU) lililokuwa likitokea Wilaya ya Muheza kuelekea Tanga Mjini na kuigonga Coaster aina ya Nissan Civilian (T 228 DPD) iliyokuwa imeharibika Barabarani katika eneo la Tanganyika, Wilayani Muheza

Akithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo Kamanda wa Polisi ACP Maket Msangi amesema ajali hiyo imetokea June 15, 2024 majira ya Saa 3 kamili usiku ambapo Jeshi linaendelea kuwasaka dereva wa wa Lori la Mizigo ambaye ni Alvis Livingston pamoja na Dereva wa Coaster aina ya Nissan Civilian ambaye Jina lake halijaweza kutambukika.

Kamanda amesema katika Ajali hiyo waliofariki ni pamoja na Anwar Juma (30) kondakta, Shabi Omari (45) abiria, Hassan Abdallah (32) na mwanamme mmoja ambaye bado jina lake halijatambulika ambae anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30.

Majeruhi katika tukio hilo ni wanne ambao ni Juma Adam, Hussein Kombo, Mundhir Mwait na Sikujua Hamid ambao hali zao ni nzuri na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali teule Muheza.

Miili ya Marehu imehifadhiwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muheza na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Kamanda amesema Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Roli Alvis Livingstone kwani alikuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo kisha kuligonga gari namba T 228 DPD aina ya Nissan Civilian hatimae kusababisha vifo na majeruhi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

AUCHO AADHIBIWA KWA KOSA LA KUPIGA ...
MICHEZO Kiungo wa klabu ya Yanga, Khalid Aucho raia...
Read more
13 BEST REASON WHY HUMILITY IS IMPORTANT...
It makes you easy to be corrected and to grow
See also  Atlético Madrid enter the race for Gallagher
It...
Read more
WANAODHANIWA KUTAKA KUMUUA MBUNGE CHRISTOPHER OLE-SENDEKA
HABARI KUU Watu wasiojulikana wamemfyatulia risasi zisizopungua nne Mbunge wa...
Read more
KAULI YA GAVANA EMMANUEL TUTUBA YAWAKERA WATANZANIA
HABARI KUU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba...
Read more
Issa Hayatou Afariki Dunia
Rais wa zamani wa shirikisho la soka barani Afrika CAF...
Read more

Leave a Reply