Mwijaku atakiwa kulipa shilingi bilioni 5 kwa kumchafua Masoud Kipanya

0:00

Wakili wa Masoud Kipanya mtangazaji maarufu ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa kupitia vibonzo, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates amesema mteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa na kauli za Mwijaku juu yake mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya nae kazi

“Masoud anaona aibu hata kutembea mbele ya watu, tuhuma za kujihusisha na biashara haramu zimemuathiri”

Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au kulipa faini ya shilingi bilioni 5 za Kitanzania

Awali, hivi juzi kati baada ya Mwijaku kuhama kutoka Clouds FM kwenda Crown FM, Masoud Kipanya alitoa maoni yake kuhusu hilo, lakini Mwijaku alionekana kutopendezwa

Mwijaku aliibuka kudai kwamba Masoud Kipanya anajihusisha na biashara haramu Hili ndio chapisho la Mwijaku kuhusu Masoud Kipanya ndilo limeleta shida hadi kutakiwa kulipa fidia ya Tsh Bilioni tano.

✍Kaka nikuombe kitu hebu niache ndugu yangu. Hujui maisha yangu na hujui nilipo tokea. Mpaka hapa nilipo, Na kama umetumwa pia nawaonya woote. NIACHENI Wewe wakati unajitafuta kimaisha ulifanya vingi hadi MATANGAZO YA POMBEE hakuna Muislamu walie kunyooshea kidole walikaa kimya sababu hatujui ULIPITIA kitu gani katika maisha yako.

✍Instead ya kuanza kufatilia maamuzi yangu. Hebu kaa utubu dhambi zakoo za kufanya matangazo ya Pombe na kuwashawishi mamilioni ya watanzania kuharibu maisha yao Mimi nakuomba uniache hujui shida zangu hujui nimekujaje mjini? Au unataka woote tufanye biashara haramu kama unazo zifanya wewe? Wengine hatuwezi kufanya biashara HARAMU kama wewe mzee Usitake tuseme mambo yako hapa tukaharibuana usiku huu.

✍Mimi natafuta hela yangu ya halali mzee sijawahi kula pesa ya haramu kama wewe. Na kaa ukijua sihitaji ushauri katika maisha yangu.

✍Kaa utubu zambi zako na hayo mabiashara yako ya kiharamu mzeee laiti watanzania wangejua unayo yafanya sidhani kama kuna mtu angeketi kukaa na wewe au hata kuzungumza na wewe. Umekua mwiba kwa vijana kuharibikiwa maisha yao, na hakuna alie simama na kukumyooshea vidole #

✍Leo Mil 20 inafanya mshipa unakusimama kama umetolewa roho kaka . Haya maisha kila mtu ana muda wake mzeee. Wewe muda wako ulipita na uliamua kutangaza pombe na kujiingiza kwenye ma biashara yako haramu hakuna alie kusema wala kukushauri ,so tuache tulio chagua njia halali na salama kaka Chini ya ardhi ya mola wetuu.

✍Niache narudia tena nitayasema yako yoote uje useme nimekuharibia maisha kaka yangu. Nakuonya achana na mimi kabisaaa. Kama ulizoe kuwazodoa viongozi wa nchi na maraisi kwa kuwadhalilisha sio mimi sitakaaa kimyaaaaaaa. JIJESHIMU hujui nimefikaje hapa.

✍Ungekua wewe mtangazaji bora usinge kubali KUHONGWA ili uiseme vibaya serikali na viongozi wake.

✍Na unajua kabisa ni kosa kutumika hivyo, Na watu tumekaa kimyaa kabisa na serikali imeamua kukupuuza sasa unaona huko hapatoshi unanifata na mimi, Kaka yangu RESPECT ME sitakaa kimya.” Mwijaku.

See also  The Al Nassr player announced the launch of his new YouTube channel “UR Cristiano” with eight short videos on Wednesday.

Jana, Mwijaku aliitisha mkutano na waandishi wa habari kumuomba msamaha Masoud lakini leo Masoud Kipanya nae ameitisha mkutano na waandishi

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Protest: ‘Arrest Peter Obi, see what’ll happen’...
Popular Nigerian entertainer, Charles Oputa, popularly known as Charly Boy,...
Read more
EVERTON YAPUNGUZWA ALAMA 10 SABABU HIZI ...
MICHEZO Klabu ya Everton imekatwa alama 10 kwenye ligi kuu...
Read more
QUALITIES OF A GOOD MARKETING EXPERT
Strategic thinking: A good marketing expert is able to think...
Read more

Leave a Reply