Klabu ya Yanga itaweka kambi yake ya maandalizi nchini Urusi ambapo itakuwa wageni wa klabu ya CSKA Moscow walioingia nao ushirikiano.
Hii itakuwa mara ya kwanza Kwa klabu ya Yanga kwenda kuweka Kambi nje ya nchi hasa huko Urusi kwani Kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikiweka kambi yake katika eneo lao la siku zote la AVIC TOWN na kuchukua ubingwa misimu mitatu mfululizo.
Klabu ya Yanga na CSKA Moscow ziliingia makubaliano ya ushirikiano utakaoifanya Yanga kupeleka wachezaji wa timu ya vijana wenye vipaji.
Hivyo Kwa kuanzia ni hapa katika kipindi Cha Pre season na Yanga itaweka kambi huko na tayari wameshaanza kutengeneza mchakato wa safari hiyo Kwa kuwaombea visa wachezaji.
“Rais wetu alishaweka wazi katika mkutano mkuu wikendi iliyopita, tuna mialiko sehemu tatu,Afrika Kusini tumealikwa na Kaizer Chiefs baada ya kuwaalika katika kilele Cha wiki ya mwananchi, Kenya tulipokea mwaliko wa Raila Odinga na pia tuna mwaliko wa Ulaya, hivyo ni wazi msimu huu tutakuwa nje ya nchi”, amesema Ali Kamwe.
.