Ifahamu Eid Al-Adh’haa au Sikukuu Ya Kuchinja

0

0:00

Ikiwa leo ni siku ya Waumini wa dini ya Kiisalam wakiadhimisha Sikukuu ya Eid Ul Adh’haa au ‘Sikukuu ya kuchinjaā€™

Tuifahamu siku hii maalum ni siku gani hasa!!

Sikukuu hii huashiria kuisha kwa ibada ya Hija eneo la Mina, nchini Saudi Arabia, lakini huadhimishwa na Waislamu duniani kote kama ishara ya kumbukumbu ya imani aliyoionyesha Nabii Ibrahimu (AS).

Eid Al-Adha huanza siku ya kumi ya Dhuā€™l-Hijja, mwezi wa mwisho kwenye kalenda ya Kiislamu, na hudumu kwa muda wa siku nne. Huanza baada ya siku ambayo Waislamu kumaliza ibada ya Hija wakishuka kutoka katika Mlima wa Arafah.

Sikukuu hii husherehekewa na Waislamu duniani kote, kama zilivyo tamaduni za imani ya dini nyingine.

Lakini Eid Al-Adh’haa ni nini?

Historia ya Eid. Eid Al-Adha, ni sikukuu ya Kiislamu inayoadhimishwa kukumbuka tukio la Nabii Ibrahimu (AS) kuwa tayari kumtoa sadaka mwanaye wa pekee Ismail (AS), kwa kumchinja kama alivyoagizwa na Mwenyezi Mungu . Ingawa alikuwa ni mtu mwema na aliyempenda mwanawe; imani yake na kujitoa kwa Mungu vilikuwa na nguvu zaidi kiasi ambacho angeweza kufanya chochote alichoagizwa.

Kitendo cha utayari wa Nabii Ibrahimu kumtoa sadaka mwanaye wa pekee kwaMungu kilipelekea Mungu kutoruhusu kuchinjwa kwa mtoto yule na badala yake akampatia mwanakondoo kuwa mbadala.

Kitendo cha kuchinja mnyama. Kwa wengi walio nje ya imani ya Kiislamu wamekuwa wakilitafsiri hili tukio tofauti. Kinyume chake, Waislamu huwachinja wanyama wao kwa kutanguliza sala kwanza na kuwachinja kwa jina la Mungu, ambaye amewapa mamlaka juu ya wanyama hao na haki ya kuwala. Hata hivyo, Wailsamu wanapolitaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, ni kutukumbusha kwamba uhai ni kitu kitakatifu. Kwa hiyo kiuhalisia, hukifanya kitendo hiko kwa kumbariki mnyama na kumshukuru Mungu, pamoja na kutambua utakatifu wa maisha ya mnyama.

See also  CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU),kimemjia juu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya matamshi aliyoyatoa dhidi ya Mtumishi wa umma wilayani Longido, kikidai kitendo hicho kinavunja heshima ya mfanyakazi,Kudhalilisha na kuvunja hali na morali ya kufanya kazi.

Nyama hugawiwa kwa familia, jamaa na maskini. Eid Al-Adha pia hujulikana kama ā€˜Sikukuu ya Kuchinja.ā€™ Kondoo, ngā€™ombe, mbuzi, au ngamia ni sadaka kwa jina la Mwenyezi Mungu. Nyama itokanayo na sadaka hugawanywa katika mafungu matatu: theluthi moja kwa ajili ya familia, theluthi nyingine kwa marafiki na majirani, na theluthi inayobakia hugawiwa kwa maskini.

Eid Mubarak.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading