Mpango amwakilisha Rais Samia Kwenye Mazishi ya Saulos Chilima

0:00

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Kitaifa ya Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Saulos Chilima aliyefariki dunia katika ajali ya ndege.

Ibada ya mazishi hayo imefanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi.

Akitoa salamu za rambirambi Dkt. mpango amesema Tanzania inatoa pole na kuungana na waombolezaji wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Hayati Chilima alikuwa kiongozi imara, mwanamajumui wa kweli wa Afrika ambaye wakati wote alitanguliza mbele maslahi ya wananchi anaowaongoza na Afrika kwa ujumla.

Pia amemtaja Hayati Chilima kama kiongozi aliyesimamia umoja, amani na usalama, mageuzi ya kiuchumi ya Malawi na utawala wa kidemokrasia nchini Malawi.

Makamu wa Rais amesema wananchi wa Malawi na Ukanda wote kwa ujumla wanapaswa kumuenzi Hayati Chilima kwa kuendeleza yale aliyosimamia na kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Ipswich Town legend and former Scotland manager...
The ex-Scotland defender, who managed the national team from January...
Read more
JKT IPO MBIONI KUACHANA NA MATUMIZI YA...
HABARI KUU "JKT TUKO TAYARI KUTEKELEZA, MATUMIZI YA NISHATI SAFI...
Read more
WASAGAJI HAPA MTASUBIRI SANA
Alisha Lehman Raia Wa Uswisi Pamoja Mpenzi Wake Douglas Luiz...
Read more
Actress Bisola Aiyeola shares her reasons for...
Bisola Aiyeola, a well-known actress and public figure from Nigeria,...
Read more
Spurs to appeal length of Bentancur's ban...
Tottenham Hotspur will appeal against the length of Rodrigo Bentancur's...
Read more
See also  WIVES WHO CAN'T HANDLE THE TRUTH

Leave a Reply