Fahamu Sababu za Mimba Kuharibika

0:00

9 / 100

AFYA

Mimba kuharibika ni kitendo cha mwanamke kupoteza mimba au ujauzito, na mala nyingi hali hii hujitokeza ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito.

Ingawa watu wengi wamekuwa na imani mbalimbali kwamba kuharibika kwa mimba huchangiwa na ushirikina, Jambo ambalo sio sahihi kabisa, kwani kuharibika kwa mimba husababishwa na mambo mbali mbali yanayoathiri ufanyaji kazi wa mwili na afya ya mtu kiujumla.

Fahamu sababu zinazoweza Kupelekea Mimba kuharibika;

1️⃣. Hitilafu za kijenetiki ( Hitilafu za vinasaba ); Ikiwa wakati wa urutubishaji namba au mpangilio kwa kromosomu utakaa tofauti na mpangilio wa asili kwaajili ya uzalishaji basi mimba itaharibika.

2️⃣. Maambukizi ya vijidudu wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua. Vijidudu hivyo huambatana na magonjwa kama Rubella, kaswende, hepesi n.k ambayo ni hatarishi ya mimba kuaribika.

3️⃣. Hitilafu katika mfumo wa homoni; Homoni husaidia mwili kuwasiliana na kufanikisha zoezi la kukamilika kwa mimba mpaka mtoto kuzaliwa, inapotokea changamoto katika mfumo huu wa homoni ni dhahiri mama mjamzito anaweza kupoteza mimba yake.

4️⃣. Matumizi ya sigara na pombe pia humweka mama mjamzito hatarini kupoteza au kuaribu mimba yake.

5️⃣. Kwa wagonjwa wa Sukari, sukari isiporatibiwa pia huweza kuleta hatarishi ya mimba kuharibika na magonjwa kama shinikizo la juu la damu.

Nini kifanyike.?!
Kuharibika kwa mimba kunaweza kutokea kwa wakati wowote ule kutokana na sababu tajwa hapo juu au nyinginezo zozote, lakini kujikinga na hii hali ni vyema kufanya mambo yafuatayo;

1️⃣. Kwa wapenzi ni muhimu kumwona daktari ili kujua hali za kijenetekia kabla ya ndoa.

See also  BUSINESS IS A BATTLEFIELD: Strategies for Success

2️⃣. Kwa mama pale atakapoona dalili za ujauzito ni muhimu kupata ufatiliaji na uangalizi wa karibu kutoka kwa daktari, ili kuepusha changamoto zinatozoweza kujitokeza njiani.

3️⃣. Kwa wagojwa wa sukari ni muhimu kufanya uratibu wa sukari chini ya uangalizi wa daktari.

4️⃣. Kwa mama mjamzito ni muhimu kufanya mazoezi kama yoga ili kuimarisha mzunguko wa damu na afya kiujumla.

5️⃣. Kula mlo kamili wenye virutubisho vyote kama asidi ya foliki.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mexico dominate US in 2-0 friendly win
Mauricio Pochettino suffered his first defeat in only his second...
Read more
WALIOLIPUA KANISA LA OLASITI ARUSHA KUNYONGWA
HABARI KUU Masheikh 9 miongoni mwa walioshikiliwa kwa zaidi ya...
Read more
French authorities have opened an investigation into...
Jolly filed a complaint after receiving threats and online attacks...
Read more
RAIS LUIS RUBIALES KUFUNGWA JELA KWA KOSA...
MICHEZO Waendesha mashtaka nchini Uhispania wametaka aliyekuwa Rais wa Shirikisho...
Read more
MAMBO MAKUU 4 YA KUZINGATIA KABLA YA...
MAPENZI Fahamu mambo 4 muhimu unayopaswa kuyazingatia uwapo chumbani na...
Read more

Leave a Reply