HABARI KUU
Mamia ya mahujaji wamefariki dunia na maelfu wanatibiwa kutokana na magonjwa yanayotokana na joto kali walipokuwa wanatekeleza ibada ya kila mwaka ya Hija mjini Makkah, Saudi Arabia, huku joto likifikia nyuzi 49 (Fahrenheit 120).
Wakati CNN ikisema waliokufa ni mamia, India Today imetaja zaidi ya 1,000 na The Guardian la Uingereza limetaja watu 550.
Kwa mujibu wa CNN, Waindonesia 165 ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia, Wajordan 41, Watunisia 35 na Wairani 11.
Taarifa ya CNN inasema raia wengine 22 wa Jordan hawajulikani walipo na Wairani 26 wamelazwa hospitalini.
Chanzo: Mashirika mbalimbali ya habari
India Today imesema miongoni mwa waliokufa ni Wamisri 650. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya Watanzania kuhusiana balaa hilo.